News
Maajabu Loliondo Pt. 1
Tangu jadi wachungaji na wahubiri na baadhi ya wanaojiita manabii wamekuwa wakidaiwa kufanya yale ambayo yameshindikana kufanyika kupitia sayansi ya kisasa. Yaani kuponya wagonjwa kwa kumshika kwa mkono, au kupigwa na upepo au kwa kutumia njia ya ajabu. Lakini ni wachache kama wapo ambao wanaponya kwa imani. Katika miezi michache iliyopita maelfu ya watu wa matabaka tofauti wanamiminika katika kijiji kimoja kaskazini mwa Tanzania ili kupata kikombe cha dawa kutoka kwa aliyekuwa mchungaji wa Kanisa la Lutheran, Ambilikile Mwasapile. Mzee huyo wa umri wa miaka 72 anasema kuwa anaweza kutibu magonjwa sugu kama ukimwi, saratani na hata kisukari. John-Allan Namu ambaye amerejea ameandaa sehemu ya kwanza ya makala yafuatayo ya maajabu loliondo ambayo yamesomwa na Rashid Abdallah.
1200 PM Live
1300 NTV at 1
1400 Until Forever
1530 Cartoon Network
1600 NTV at 4
1700 The Beat
1800 Mara Clara
1900 NTV Jioni
1930 Beautiful But Unlucky
2030 Demigods
2100 NTV Tonight
2150 The Hostel
2230 Little Star
