NTV Jioni

Msanii na Sanaa: Habel Kifoto

Tuesday August 2, 2011

Share Bookmark Print Email Rating

Alternative text.
Msanii na Sanaa: Habel Kifoto...

Na katika makala ya Msanii na Sanaa tunakuletea kumbukumbu ya msanii mashuhuri wa humu nchini kutoka Taita Taveta, marehemu Habel Kifoto. Alikuwa muasisi wa bendi ya jeshi ya Maroon Commandos na alifariki akiwa ni mwenyekiti wa chama cha kutetea haki za wanamuziki wa Kenya.

Share This Story
Share

0 Comments
Login Not a member?  Register here

You need to login first to submit a comment.

Maajabu Loliondo Pt. 2

Wednesday March 23, 2011

Share Bookmark Print Email Rating

Alternative text.
Maajabu Loliondo Pt. 2...

Mimi si mganga wa kienyeji,ninatibu kwa miujiza ya mungu. Hayo ni maneno ya mchungaji Ambilikile Mwasapile ambaye amekuwa kivutio cha wengi kutokana na dawa yake inayotibu magonjwa sugu kama ukimwi na saratani huko Loliondo nchini Tanzania. Hata hivyo Ambilikile anasisitiza kuwa kupona kwa mgonjwa kunategemea imani yake. Inafuata sasa sehemu ya mwisho ya makala maalum ya Maajabu Loliondo.
Tunaarifiwa kuwa mchungaji huyo Ambilikile Mwasapile atabadilisha eneo la utoaji dawa. Ambilikile anapanga kwenda katika eneo lenye nafasi kubwa kwani watu wanazidi kumiminika katika makaazi yake kijijini Samunge.

Share This Story
Share

1 Comments
Login Not a member?  Register here

You need to login first to submit a comment.

Submitted by tonyngache
Posted March 23, 2011 11:55 PM

loliondo pt 2 is seen to be more than a miracle !!!

Maajabu Loliondo Pt. 1

Tuesday March 22, 2011

Share Bookmark Print Email Rating

Alternative text.
Maajabu Loliondo Pt. 1...

Tangu jadi wachungaji na wahubiri na baadhi ya wanaojiita manabii wamekuwa wakidaiwa kufanya yale ambayo yameshindikana kufanyika kupitia sayansi ya kisasa. Yaani kuponya wagonjwa kwa kumshika kwa mkono, au kupigwa na upepo au kwa kutumia njia ya ajabu. Lakini ni wachache kama wapo ambao wanaponya kwa imani. Katika miezi michache iliyopita maelfu ya watu wa matabaka tofauti wanamiminika katika kijiji kimoja kaskazini mwa Tanzania ili kupata kikombe cha dawa kutoka kwa aliyekuwa mchungaji wa Kanisa la Lutheran, Ambilikile Mwasapile. Mzee huyo wa umri wa miaka 72 anasema kuwa anaweza kutibu magonjwa sugu kama ukimwi, saratani na hata kisukari. John-Allan Namu ambaye amerejea ameandaa sehemu ya kwanza ya makala yafuatayo ya maajabu loliondo ambayo yamesomwa na Rashid Abdallah.

Share This Story
Share

0 Comments
Login Not a member?  Register here

You need to login first to submit a comment.

Gumzo Mitaani: Ukabila na ufisadi Kenya

Wednesday February 23, 2011

Share Bookmark Print Email Rating

Alternative text.
Gumzo Mitaani: Ukabila na ufisadi Kenya...

Imesemwa kwamba ukabila na ufisadi ndio adui wa maendeleo. Mambo mengi hayatekelezwi kwa njia inayostahili kutokana na maovu hayo ya kijamii na ingawa kuna tume za kukabiliana na hayo athari zake hazikosi kuonekana kila siku hapa nchini. Wakaazi wa Kabarnet Baringo wanazungumzia hilo katika kikao cha gumzo mitaani.

Share This Story
Share

0 Comments
Login Not a member?  Register here

You need to login first to submit a comment.

Msanii na Sanaa: Mlinzi wa mheshimiwa

Wednesday February 23, 2011

Share Bookmark Print Email Rating

Alternative text.
Msanii na Sanaa: Mlinzi wa mheshimiwa...

Wasanii wengi hupata msukumo wa kuendeleza vipawa na kazi zao kutokana na matukio ya kweli maishani mwao. Mmoja wao ni Afande Ben ambaye mchumba wake alimtoroka alipokuwa katika chuo cha mafunzo ya polisi. Msanii huyo alitunga wimbo kuhusu kisa hicho baada ya kumaliza mafunzo yake na sasa ni msanii huku akiwa ni mlinzi wa mheshimiwa mbunge wa Budalang’i Ababu Namwamba.

Share This Story
Share

0 Comments
Login Not a member?  Register here

You need to login first to submit a comment.

Ni uganguzi au wizi?

Sunday January 23, 2011

Share Bookmark Print Email Rating

Alternative text.
Ni uganguzi au wizi?...

Kulikuwa na hekaheka katika kiwanda cha kusaga nafaka cha Kabansora hapa jijini Nairobi wakati waganga walipoitwa kutatua kesi ya wizi katika kampuni hiyo. Tairi za thamani ya shilingi milioni moja unusu zilitoweka na wakati wasimamizi wa kiwanda waliposhindwa kumtambua mwizi wakawaita waganga kuwasaidia.

Share This Story
Share

0 Comments
Login Not a member?  Register here

You need to login first to submit a comment.

Nzambani: Jiwe la ajabu Kitui

Monday October 4, 2010

Share Bookmark Print Email Rating

Alternative text.
Nzambani: Jiwe la ajabu Kitui...

Kuna mengi ya kihistoria ambayo hayajaangaziwa kikamilifu katika maeneo mbalimbali ya humu nchini. Moja ya maeneo hayo ni jiwe la nzambani kiungani mwa mji wa Kitui. Kuna jiwe moja ambalo inadaiwa ukilizunguka mara saba utabadilika maumbile yakjo ya kijinsia. Lolani atuarifu zaidi.

Share This Story
Share

0 Comments
Login Not a member?  Register here

You need to login first to submit a comment.

Mbitini Kamuti special

Monday October 4, 2010

Share Bookmark Print Email Rating

Alternative text.
Mbitini Kamuti special...

Kila yakitajwa mambo ya uchawi jimbo la Kitui huongoza lakini ukweli wa jambo hilo haujawahi kuthibitishwa. Kuna wengi huenda Kitui kutafuta hata dawa za mapenzi. Lolani Kalu alisafiri hadi Mbitini na kukutana na mganga mmoja maarufu katika eneo hilo ambaye inaaminika hukabiliana vilivyo na athari za uchawi.

Share This Story
Share

0 Comments
Login Not a member?  Register here

You need to login first to submit a comment.

Usiku wa raha Kitui

Monday October 4, 2010

Share Bookmark Print Email Rating

Alternative text.
Usiku wa raha Kitui...

Kulikuwa na shamrashamra za mwisho wa wiki katika mkahawa wa riverside mjini kitui wakati wa shindano la kusisimua la kucheza densi. Mihemko ilikuwa ya hali ya juu kama anavyotuarifu Lolani Kalu.

Share This Story
Share

0 Comments
Login Not a member?  Register here

You need to login first to submit a comment.

Upekuzi: Makala ya ndoto languzi pt. 3

Friday September 24, 2010

Share Bookmark Print Email Rating

Alternative text.
Upekuzi: Makala ya ndoto languzi pt. 3...

Katika hitimisho la Ndoto Languzi katika makala ya upekuzi Mustafa Mwalimu anaangazia jinsi polisi wanavyochangia kuendelea kudumu kwa biashara haramu ya ulanguzi wa watu. Aidha Mustafa na mwenzake Yassin Juma walikamatwa na polisi walipokuwa wakiwaandama Waethiopia waliokuwa wakisafirishwa kutoka Moyale hadi Nairobi.

Share This Story
Share

0 Comments
Login Not a member?  Register here

You need to login first to submit a comment.

Today's Schedule
February 9, 2012

1200 PM Live
1300 NTV at 1
1330 MoreThan Love
1500 Cartoon Network
1600 NTV at 4

1630 Unfabulous

1730 The Beat
1800 Rivals
1900 NTV Jioni
1930 Beautiful But Unlucky
2030 Mali
2100 NTV Tonight
2200 Extreme Makeover: Home Edition


Today's Highlights